TENGENEZA ULIMWENGU WA MTOTO WAKO
Mch. Upendo Epafrodito
Mithali 22:6, Mathayo 7:1-5
Utangulizi.
Ulimwengu kwa ujumla ni nchi mbalimbali zilizopo duniani. Lakini kwa muktadha wa somo la leo, ulimwengu wa mtoto ni jumla ya khali ya masiha ya mtoto kimwili, kimtazamo, kihkali na kiakili.
Hivi ni vile mtoto anaweza kukutana na jambo na kukabiliana nalo. Khali ya namna ambavyo mtoto anakabiliana na mambo mbali mbali ni khali inayotengenezwa wala haiji kwa ghafla au Bahati.
Vile mzazi afanyavyo mambo ndivyo inavyoathiri Maisha ya mtoto na kutengeneza ulimwengu wake kulingana na namna mzazi wake ameishi. Uwepo na neema ya Mungu ni halisi lakini hauondoi wa wazazi kutengeneza masiha ya Watoto wao.
Katika kitabu cha mathayo 7:1-5, tunaona Yesu akiwasema wayahudi ambao walikuwa wanaona matatizo ya wenzao bila kuangalia matatizo yao binafsi. Swala hili lipo kwa wazazi wengi sasa ambao wanaona matatizo ya Watoto wa wenzao bila kujua kama Watoto wao binafsi wana matatizo.

JINSI GANI TUNAWEZA KUTENGENEZA ULIMWENGU WA WATOTO WETU?
- Kwa kuwaombea Watoto.
Kuwaombea Watoto kuhusiana na Maisha yao, mzazi ana mchango wa kuendeleza Maisha ya Watoto wao kwa kuwaombea. Maombi huumba ulimwengu wa mtoto.
- Kutamka/ Kutangaza ahadi za Mungu juu ya Maisha ya Watoto.
Kuna ahadi nyingi za Watoto katika biblia na ni muhimu wazazi kumtamkia mtoto wako ahadi zilizowekwa kwaajili katika neno. Vile vile kuna ahadi za ujumla ambazo si kwa mtoto kimaalum lakini zinaweza kujenga ulimwengu wao.
- Muelekeze mtoto mamabo ya ufalme.
Usalama wa ulimwengu wa mtoto unakuwepo pale tunapo washirikisha katika agenda za kiMumngu. Mzazi anapswa kuwa mfano bora katika hili eneo. Wazazi wawashirikishe Watoto agenda za KiMungu husasani zile wanazojihusha nazo wenyewe.
- Ishi unachokisema.
Watoto hujifunza sana katika tunachosema na tunachoongea mara zote. Hivyo kila tunaposema jambo kama wazazi au walezi, lazima tuhakikishe kufanya vzr ili kuwafundisha Watoto wetu.
- Malezi ya ufuatiliaji
- Kumadabisha
Hii inahusha pia kumkatalia baadhi ya mambo. Mtoto ajifunze kwamba kuna kukataliwa katika baadhi ya mambo.
Hitimosho
Wazazi tunaweza kuwa chanzo cha kujenga ulimwengu mzuri kwa Watoto wetu au wale Watoto tutakao kuja kuwa nao.

