SOMO: VIKWAZO VYA KUTUZUIA KUENEA – PASTOR IGNAS MPUNGA

MGI SERVICE – 04/02/2024

MHUBIRI: PASTOR IGNAS MPUNGA

SOMO: VIKWAZO VYA KUTUZUIA KUPANUKA NA KUENEA

  • UVIVU

Mithali 13: 4 Nafsi ya mtu mvivu hutamani asipate kitu; Bali nafsi ya mwenye bidii itanenepeshwa.

“Mvivu hana Macho ya Kuona Fursa.” Pastor Ignas Mpunga

Wanaofanikiwa ni Wenye Bidii.

Moja ya Dalili za Umasikini ni Kuishia Umezeeka Ukiwa bado Umeajiriwa.

Mwanzo wako sio mwisho wako, anza na kidogo Mungu atakuinua kwenda hatua kubwa Zaidi.

  • ROHO/TABIA YA KUTOKUJALI

Kutokujali ni kutokuzingatia au kuondoa uthamani kwenye vitu vya msingi vya kwenye maisha (kupuuzia).

Mwanzo 25: 29-34 Esau Anadharau/anapuuzia/hajali haki yake ya mzaliwa wa kwanza. (32- Esau akasema, Tazama, mimi ni karibu kufa, itanifaa nini haki hii ya uzazi?)

Dalili za Mtu Mwenye Roho ya Kutokujali:

a/ Sio mtu wa Kushughulikia Vitu Vinavyokukwamisha kwenye Maisha Yako.

b/ Kutokujisikia kuwajibika kwenye jambo linalokukwamisha.

c/ KUISHI MAISHA YASIYO NA TAHADHARI

Mtu asiye na tahadhari hana tabia ya kuweka akiba ya fedha anazopata.

d/ TABIA YA KUAHIRISHA MAMBO

e/ Kupunguza viwango vinavyotakiwa.

Kutokuvipa thamani inayostahili vitu kwenye maisha yako.

Daniel 1:8 Lakini Danieli aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme, wala kwa divai aliyokunywa; basi akamwomba yule mkuu wa matowashi ampe ruhusa asijitie unajisi.

  • KURIDHIKA NA MATOKEO MADOGO

2 WAFALME 13:14-19

Wafilipi 3:8-15

Sababu za Watu Kuridhika na Vidogo

a/ Kuogopa kulipa gharama

b/ Hofu ya Kuanza jambo Jipya

c/ Kuzoea mifumo ya kizamani.

Ili uweze kupanua mipaka na kuenea mwaka 2024 unatakiwa uende hatua ya ziada. Usikubali kufanya vitu kwa viwango vya chini.

Usiridhike na matokeo madogo, weka malengo makubwa na yafanyie kazi kila siku ili yaweze kutimia. Usikubali hata kidogo kufanya mambo ya kawaida ambayo yanashusha viwango vyako na vya Mungu alieko ndani yako.

Acha uvivu, Jali Mambo ya Msingi, na usikubali kuridhika na Matokeo Madogo.

“MWAKA 2024 NI MWAKA WA KUPANUA MIPAKA NA KUENEA.”

Karibu kwenye Ibada

Mountain of Glory International – MGI,

MBEZI BEACH AFRICANA

Ratiba za Ibada:

Ibada ya Kwanza (ENGLISH SERVICE): 7:00AM – 09:00AM

SHULE YA UANAFUNZI: 09:00AM-10:00AM

IBADA YA PILI (SWAHILI SERVICE): 10:00AM – 12:30PM

Simu: +255 784 862 273

Website: www.mgi.or.tz

Email: info@mgi.or.tz

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *